Monday, May 28, 2012

MINDSET - 1 aka MTAZAMO or MTIZAMO una umuhimu gani?









Habari Wadau,


Hapo kabla niliomba udhuru kutokana na Bongo Pix Blog
kutokuwa na daily updates kama ilivyozoeleka tangu kuanzishwa kwake yapata
miaka sita sasa, hii ni kutokana na mambo mbalimbali na mengi yakiwa nje ya
uwezo wangu (DARASA),  lakini pia na
jukumu la kuifanyia mabadiliko makubwa blog hii, ili kuendeleza libeneke la
kuelimisha, kuhabarisha, kuburudisha na hata kuonya pia.





Kwa kipindi cha karibia mwaka BWANA aliniteua na kunipeleka “DARASANI”,
sijui aliona nini kwangu mimi mtu nisiyefaa, hata kunipa upendeleo huu, mimi
sijui bali, twaambiwa “niliteuliwa kabla ya kuumbwa tumboni mwa mama yangu”,
Darasa hili si la kawaida, wengine uliita majaribu au mitihani ya Mwenyezi
Mungu, vyovyote itakavyokuwa si darasa la kawaida, nashukuru sana Mungu kwa
kuniteua na kunipitisha katika darasa lake.  Twaambiwa “sio sisi tuliomchagua, bali ni yeye
alitupenda sisi akatuchagua”





Darasa halikuwa rahisi, napengine kama Bwana angeniambia
kabla kuwa nitapitia darasa hili pamoja na kunionesha “MASOMO” ambayo
nitajifnza na kufaulu, maana lazima ufaulu, nadhani kibinadamu ningekataa,
ndio, course outline haikuwa ya mchezo, lakini nashukuru Mungu ameniwezesha na
sasa mimi ni MSHINDI.








Nimejifunza mambo mengi mno katika kipindi chote hicho, na
panapo majariwa tutashirikishana hapa hapa jamvini baaadhi ama yot niliyojifunza,
nina hakika kuwa hii itasaidia ama kufungua watu wengine pia, ambao pengine nao
wako darasani au uenda wakaingia darasani, iwapo watachaguliwa naye.





Moja ya vitu nimejifunza ni kumtegemea Mungu 100% katika
maisha yetu, ikiwa wataka mafanikio, kuinuliwa, utajiri, uponyaji au chochote
maishani, NENO lake liko wazi kabisa juu ya hayo yote, kwa maana anatuwazia
mawazo yalioyo mema, kutupa sisi tumaini siku zetu za mwisho, hivyo tukijifunza
kumtumaini yeye asilimia mia moja, yeye naye anatenda sawa na neon lake.





Katika Darasa hili nilijifunza pia kitu inaitwa MINDSET, (MTIZAMO,
sina hakika kama tafsiri ni sahihi au kuna neno jingine) na kwanini watu wengi
hawawezi kusonga mbele au kupiga hatua stahiki sawa na mpango wa Mungu maishani
mwao kutokana tu ni hii kitu MINDSET.


Kwa tafsiri ya haraka kwa mujibu wa mitandao mbalimbali ni:-










MINDSET


1. A mindset is a set of assumptions, methods, or notations
held by one or more people or groups of people that is so established that it
creates a powerful incentive within these people or groups to continue to adopt
or accept prior behaviors, choices, or tools, 
BY WIKIPEDIA





2. The ideas and attitudes with which a person approaches a
situation, especially when these are seen as being difficult to alter.
Dictionary.com





1.     3. a)   A fixed mental attitude or disposition that
predetermines a person's responses to and interpretations of situations.


2.     b)   An inclination or a habit.   By Answers.com 





Nitajaribu kufafanua kwa undani zaidi juu ya somo hili katika post zitakazo fuata, lengo ikiwa ni kuelimishana na pengine kuna mtu anaufahamu mkubwa zaidi katika eneo ama somo hilo anaweza kunitumia barua pepe nami ktk brwebangira@gmail.com au nitwangie 0784475576 nami nitaishirikisha hapa jamvini. Mbarikiwe sana. 





No comments:

Post a Comment