Thursday, July 19, 2012

Ajali ya Mv Skagit Up date



 Katika ajali hii kulikuwa na Shemeji yangu mke wa mdogo wangu Crispin Kagimbo, Ms Amina Ali pamoja na watoto wawili, Collin (1) na Michael (5) ama Abdalah, mpaka sasa ni mwili wa mtoto huyo mdogo ndio umepatikana na kuifadhiwa, tunaendelea kufuatuilia waliobakia, twaomba Mwenyezi Mungu muweza wa yote wawe ni sehemu ya manusura, maana yeye pekee ndiye awezaye kuokoa kwa namna ya ajabu.  


























MAMLAKA ya udhibiti usafiri wa nchi kavu na maji
(SUMATRA),imesema meli ya MV Skagit iliyopata ajali visiwani Zanzibar,
iliondoka Bandari ya Dar es Salaam saa 06.05 mchana juzi ikiwa na abiria 248,
watoto 31 pamoja na mabaharia 9.










 Meli hiyo inayomilikiwa na Kampuni ya Seagul Transport, ilipata
usajili katika Mamlaka ya usafiri 
Bandari Zanzibar (ZMA)ikiwa na uzito wa meli (GRT)96.
 











Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo
Meneja Mawasiliano David Mziray, alichanganua kuwa cheti cha ubora wa meli hiyo
kilitolewa Agosti mwaka jana na kumalizika mwezi huo mwaka huu.










 “Mv Skagit ilikuwa na uwezo wa kubeba abiria 300 pamoja na
mizigo tani 26,  hivyo kulingana na idadi
ya abiria 288 walioondoka katika chombo hicho isingeweza kuleta madhara kama
hayo, ila tunawasiwasi waliongeza abiria njiani au mawasiliano ya hali ya hewa”
Kwa mujibu wa Mziray.
 Aidha, anafafanua kuwa idadi ya watu waliopoteza maisha hadi
sasa ni zaidi ya 34, majeruhi 146 wakati wengine wakiendelea kutafutwa.










 “Zoezi la uokoaji linaendelea katika eneo la tukio kwa
msaada wa Mv Flying Horse, Mv Kilimanjaro 111, Tug Bandari ya Zanzibar, KMKM,
Mv Zanzibar 1, Polisi wa majini, pamoja na Navy, hata hivyo bado taarifa sahihi
za waliopoteza maisha hazijapatikana kulingana na watu hao kuokolewa katika
mazingira tofauti” alibainisha Mziray.










 Hata hivyo alisema baadhi ya viongozi wa Sumatra wamekwenda
katika tukio hilo kwa ajili ya kushirikiana na ZMA ili kuokoa maisha ya watu
hao.



































Picha na stori kwa hisani ya mitandao mbalimbali. 



No comments:

Post a Comment