Ni noti za kwanza za Afrika Kusini kuwa na uso wa kiongozi mweusi na zinachukua mahala pa noti zilizokuwa na nyuso za wanyama na picha za viwanda.
Rais wa nchi hiyo, Jacob Zuma anasema kuwa noti hizo zilikuwa kama ishara ya shukrani kwa Mandela.
Bwana Mandela, mweye umri wa miaka 94, ni mmoja wa watu wanaoenziwa sana duniani baada ya kufungwa jela miaka 27 alipokuwa anapigana dhidi ya utawala wa ubaguzi wa rangi.
Gavana wa benki kuu Gill Marcus alikuwa wa kwanza kutumia noti hiyo kwa kununua bidhaa katika duka moja mjini Pretoria.
Alisema kuwa bwana Mandela ana furaha kuona noti hiyo.
Pia alielezea kuwa Afrika Kusini hujaribu kila baada ya miaka saba kubadili sarafu yake ya noti kwa sababu za kiusalama.
Sura ya Mandela iko upande mmoja wa noti hizo mpya wakati wanyama wakubwa watano Simba, Kifaru, Chui , Ndovu na Nyati, wakiwa upande wa pili.
Alishinda tuzo la amani la Nobel mwaka 1993 kwa sababu ya harakati zake dhidi ya utawala wa ubaguzi wa rangi na kuchaguliwa rais mwaka uliofuata kabla ya kujiondoa mwenyewe mamlakani baada ya kipindi kimoja tu cha utawala wake.
Akisifika sana kwa jina lake "Madiba", amestaafu siasa siku nyingi .
No comments:
Post a Comment