Tuesday, November 6, 2012

ARUSHA......WOMEN IN BALANCE KITCHEN PARTY GALA JUMAMOSI HII,UPO TAYARI?

Ni jumamosi hii ya keshokutwa tarehe 10 november pale Blue fame Tripple A.
Wazungumzaji wetu wa siku kutoka Dar es salaam ni Aunty Sadaka mwanasaikolojia ya jamii.

Kutoka Mombasa kenya tutakuwa na Getrude Mungai(Life Style Designer of Sex and Relationships.


Kwa kiingilio cha Tsh 30,000 tu utapata mafunzo ya kutosha kuhusu maisha katika ulimwengu wako mwanamke.Katika mahusiano,ndoa kwa ujumla wake.Naambiwa wadada wa Arusha siku nyingi wameshapata mavazi yao kwa rangi yetu ile ya chenza.
Ticket zitaanza kuuzwa ijumaa pale Triple A (M-PESA) na siku yenyewe ya shughuli mlangoni.Ticket ni chache sanaaaaaa jamani hakikisha unawahi mapema.
Shughuli itaanza saa nane mchana naambiwa wanawake wa Arusha kutembea usiku mwisho saa sita haya tutamaliza saa sita.
Chakula(dinner)na vinywaji laini vitapatikana free.
Muongoza shunguli ndio mimi mwenyewe
kama una swali au unataka kufanya booking ya ticket nipigie 0787 583132
 
Oriflame watakuwepo kukuuzia bidhaa yao ya kusafisha uke inaitwa feminelle.Na pia nawashukuru sana Brilliant Printing kwa kazi kubwa waliyofanya ya printing ya fliers,banner na roll up banner.
Halafu nataka msemaji mmoja kutoka Arusha embu pendekeza maana wewe ndio unawajua vyema wa huko ili tupate mwenyeji.Atakaetajwa sana ndie ntamchukua.
 
USIKOSE .

No comments:

Post a Comment