Monday, November 26, 2012

NI NGUMU KUAMINI KAMA '"SHARO MILLIONIARE" UMEKWENDA!!

Ilikuwa tuonane unipe wimbo wako mpya mdogo wangu,wiki iliyopita nikakuelekeza mpaka nyumbani lakini baadae ukanipigia kuniambia umechelewa imeshakuwa usiku utanifata ofisini.
Habari ya kifo chako imenistua sana sijalala kabisa kila nikishtuka natamani iwe ni habari ya kuzusha tu.Umekwenda bado mdogo sana ukiwa na ndoto nyingi na malengo mengi.Sitapenda kumkufuru Mungu bali nakuombea pumziko la milele.

Pumzika kwa amani  
Hussein Mkieti ‘Sharo Milionea watoto watakumiss sana'ooooh mama'

No comments:

Post a Comment