Monday, November 5, 2012

HUYU NDIO MISS TANZANIA 2012-2013

 Brigette Alfred kutokea Kanda ya Kinondoni (Sinza).Akiwa amewabwaga wenzake 29 waliokuwa wakiwania taji hilo.Na kujipatia zawadi yake ya Gari aina ya Noah na pesa taslim Tsh ml 8.Hongera sanaaaaa!!
Juzi watu wengi waliokuwa wakifatilia miss Tanzania walikuwa wakilaumu sana kuwa zawadi ni ndogo,na kuwa gari aina ya Noah sio zawadi ya maana kwa mrembo wetu wa mwaka huu.Ila nakumbuka zawadi iliyotangazwa awali ilikuwa ml 8 hii ya Noah ilikuja julikana siku ya shindano.Ulikiwa ukiingia kwenye mitandao ya kijamii kama facebook,twitter ndio kulichafuka.
Mie nilikuwa na swali kidogo kwa ndugu zangu watanzania.Hatujui kwa mwaka huu kamati ya miss Tanzania walikuwa na bajeti kiasi gani.Ila swali langu ni kwamba tuache kwamba kila mwaka mshindi amekuwa akizawadiwa gari.Wewe unadhani mshindi awe anapewa zawadi gani kulingana na maisha yalivyo hapa kwetu Tanzania.Pia washiriki wengi wanakuwa ndio wapo vyuoni au wamemaliza kidato cha nne au sita.Bado ni mabinti wadogo wenye ndoto na malengo mengi ya baadae.
Zawadi gani itamfaa?pengine gari tumekariri labda kuna namna tunaweza kumuwekea msingi mzuri wa kimaisha huyu binti.Tufikirie binti kama huyu baada ya hapo gari inahitajika kwenda service mara kwa mara,petrol iwepo ili gari  ikae barabarani na hana kazi inayomuingizia kipato.!!

No comments:

Post a Comment