Friday, November 30, 2012

POLE ZAMARADI KWA KUMPOTEZA MAMA

Juzi jumatano mida ya saa tatu  nikiwa nakuja kazini asubuhi Zamaradi alinipigia simu kuniomba ruhusa kuwa hataweza kuja kwenye move leo ya leo tena kwani usiku wake mama yake alizidiwa sana.Baada ya kuzidiwa wakamuwahisha hospitali ya Hindu Mandal ambapo asubuhi hiyo alikuwa akipumua kwa mashine.
Baada ya kufungua kipindi mida ya saa tatu na nusu nikakuta missed call ya Zama kwenye simu yangu.Nikasema ngoja nipige japo niko studio kujua kulikoni ndio Zama kupokea huku akilia sana ''Dina mama yangu amefariki''
Niliishiwa nguvu hata leo tena ikanipa shida kuendelea kuifanya.
Kwa muda kama mfatiliaji wa leo tena utakuwa umegundua kuna siku Zama yupo kuna siku hayupo.Muda wote huo amekuwa akimuuguza mama yake hata kabla baba yake hajafariki.Mama yake amekuwa akisumbuliwa na kansa ya kizazi kwa muda sana.Na muda wote amekuwa akipambana mpaka hiyo juzi alipoaga dunia.
Napenda kumpa pole Zama na pia kumwambia kuwa mama yake amemuacha akiamini atapambana maana Zama yeye ni wa kwanza kwa mama akifuatiwa na mdogo wake Ummy.Mama alipenda kuwa nanyi lakini safari yake ilifika mwisho.Lakini aliondoka akiamini Zama umpambanaji usisononeke sana bali simama my dear.
Nimekuwa namuona Zama anakuja kufanya segment lakini hayupo sawa ataniambia ''Dina sijalala jana mama alizidiwa tumemkimbiza ocean road,hali ya mama ni mbaya''halafu ataangua kilio na kujikaza na kufanya movie leo akimaliza atawahi hospitali.

Jana saa kumi mama yake Zamaradi alizikwa katika makaburi ya kisutu.
Zamaradi nakuombea wewe na familia kwa ujumla muweze kuzoea hali hii mpya katika maisha yenu.Msisononeke sana bali kuacha mapenzi ya Mungu yatimizwe.

No comments:

Post a Comment